SEHEMU KUU ZA KOMPYUTA

Kompyuta imegawanyika katika sehemu kuu mbili


Sehemu zinazoshikika (Hardware)

Sehemu zinazoshikika (Hardware), ni aina zote za vifaa vya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu.

Vifaa vya kuingizia vitu (Input devices)


  1.  (pia: kibodi (keyboard)
  2. Puku] au Kipanya (Mouse)
  3. Skana (Scanner)
  4. Mikrofoni (Microphone)
  5. Kamera (Camera













Sehemu zisizoshikika (Software)

Kompyuta haiwezi kufanya kazi mpaka kipatikane kitu kinachoitwa software, ambacho kinawakilisha programu zinazoendesha kompyuta. Programu hizo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili:
1. Programu za kuendeshea kompyuta (operating systems): programu hizo zinaitwa Windows, na kuna aina nyingi za Windows kulingana na toleo lake na ubora wake, kwani siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo tunapozidi kupokea programu nyingine za Windows zenye ubora zaidi kuliko zile za awali.
2. Programu za kufanyia kazi (application systems), nazo ni: Microsoft Office na Graphics design; programu hizo daima zinafanya kazi ndani ya windows, ambazo zinatumika kwa ajili ya kazi mbalimbali za uandishi na hesabu, na kazi nyinginezo za kuunda na kutengeneza picha n.k.

MFANO WA SEHEMU ZISIZOSHIKIKA
Vifaa hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho C.P.U. (kifupi cha Central Processing Unit), ambacho ni kiini cha kompyuta na ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vyote vya kompyuta na kutoa maelekezo yote.
C.P.U. ni sehemu kuu ya nguvu ya kompyuta, au kitovu cha kompyuta. Kazi za C.P.U. ni:

Kutawala (Control)

Ndani ya madhabodi (Motherboard) kinapatikana kifaa kinachoitwa Bios (kifupi cha Basic Input Output System), ambacho ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vya kuingizia na kutolea vitu. Ni vigumu kufuta au kurekebisha vitu vilivyomo ndani ya kifaa hicho kwani vinazingatiwa ni vitu vya kusomea tu na si kwa kazi nyingine.

Akili na mahesabu (arithmetic logical)

Kazi za mahesabu ni kazi zote zinazofanywa na hesabu, kama vile kutoa, kujumlisha, kuzidisha na kugawanya.

Kuanza kutumia Windows

Kabla hujaanza kutumia Windows unatakiwa kufanya mambo yafuatayo:
  • 1. Kuhakikisha waya wa umeme umeshaunganishwa kwenye kompyuta yako.
  • 2. Kufungua kompyuta kwa kutumia sehemu inayoitwa power.
  • 3. Kusubiri mpaka idhihiri sehemu inayoitwa desktop.


Post a Comment

Designed by OddThemes | Distributed by Gooyaabi Templates