


Microsoft Windows ni mfomu laini wa uchakatuaji (operating system) ambao ni wa msingi ambao hufanya kompyuta kufanya kazi na kuruhusu program nyingine nazo kufanya kazi. Aina za Windows zinazotumika ni Windows XP au Windows 7 na Windows 8.1 ambalo ni toleo la hivi karibuni
Microsoft ofisi ni seti (mkusanyiko) ya program ambazo hutumika katika kompyuta kuwawezesha watu kuandika dokumenti. Mfano Microsoft Word na Microsoft Excel ambayo hukuwesha kutengeneza mahesabu na majedwali na Microsoft PowerPoint ambayo hukuwezesha kuandaa mawasilisho (presentations).
Kwakuwa programu hizi hufanya kazi katika kompyuta, sehemu inayofuata inalenga kukupa ufahamu juu ya sehemu za kompyuta (hasa za nje) na zinavyofanya kazi.


Post a Comment